Usajili huu utahusu vyombo vya moto aina ya pikipiki vyenye magurudumu mawili au zaidi. Pikipiki  kwa ajili ya biashara zinatakiwa kubandikwa vibao vya namba ya rangi nyeupe na kwa ajili shughuli binafsi zitabandikwa vibao vya namba za rangi ya njano.

Usajili huu utafanyika katika ofisi zote za TRA   na mmiliki anatakiwa kwenda TRA na kadi halisi ya pikipiki na Tshs.10, 000/- kwa ajili ya kadi mpya.

Wito unatolewa kwa wamiliki wote wa pikipiki ikiwa ni pamoja na zile za magurudumu matatu au manne maarufu kwa jina la Bajaji, wafike katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa ajili ya kukamilisha usajili wa vyombo wanavyomiliki.